Kenya Airways Yasitisha Safari zake za Dubai

Kenya Airways Yasitisha Safari zake za Dubai

Shirika la Ndege la Kenya limesema limesitisha kwa muda safari zake za Ndege kuelekea Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) kufuatia kufungwa kwa anga la U.A.E kutokana na mashambulizi ya Iran yanayofanywa dhidi ya kambi za Kijeshi za Marekani zilizopo katika maeneo ya U.A.E na Nchi nyingine za Mashariki ya Kati “kwa kuwa hali hii inaendelea kubadilika, tutatoa taarifa mpya mara tu taarifa zaidi zitakapopatikana”

Marekani na Israel February 28 2026 zimeanzisha mashambulizi makubwa ya kijeshi dhidi ya Iran ambapo ndege za kivita na makombora zilishambulia Miji na Vituo vya kijeshi Nchini Iran ikijumuisha maeneo ya Tehran na sehemu nyingine za Nchi ambapo Marekani imeeleza kwamba operesheni hiyo inayojulikana kama “Operation Lion’s Roar” inalenga kupunguza tishio la nyuklia na kuzuia uwezo wa Kijeshi wa Iran ambao inauona kama hatari kwa usalama wake.

Iran imeiita hatua hiyo kama uvamizi usio na msingi na ukiukwaji wa sheria za kimataifa ambapo licha ya na kutoa wito kwa Umoja wa Mataifa kushughulikia hali hiyo imejibu kwa mashambulizi ya kulipiza kisasi kwa kurusha makombora na mashambulizi mengine dhidi ya nyenzo za Marekani na Israel katika maeneo ya Ghuba ya Uajemi, ikilenga Vituo vya kijeshi vilivyo chini ya ushirikiano wa Marekani.

Makombora yameripotiwa kulenga misingi ya Marekani katika Qatar, Kuwait, Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain kitendo ambacho baadhi ya Mataifa ya Kiarabu yamelalamikia uvamizi wa mipaka yao huku hali hii ikipelekea wasiwasi mkubwa wa kuenea kwa vita katika eneo lote la Mashariki ya Kati na kuathiri usalama wa Raia pamoja na Uchumi wa kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button