“Kilichotokea Hakikutarajiwa” Rais Samia
"Kilichotokea Hakikutarajiwa" Rais Samia
“Tunajua Ni mzigo mzito tumewapatia lakini kwa sifa zilizotajwa hapa tunajua mtaweza kwenda kuutekeleza uundwaji wa tume hii ni kuendana na sheria ya tume za Uchunguzi ya mwaka 2023 sasa kwenye hili lililotokea nimeona kabla sijaletewa tume kutoka nje tuwe na tume zetu ya ndani ifanye kazi na za nje zikija zitakuja kuzungumza na tume mwenzao ambao tayari walianza hiyo kazi”
“Kwa ufupi kilichotokea hakikutarajiwa kitokee ndani ya nchi yetu kwa sababu ya historia tuliyonayo ya usalama na utulivu wa Kisiasa ndani ya nchi hata kama kuna vipindi hatuna usalama wa kisiasa lakini haikufikia kiasi hichi kilichofikia kwa hiyo tume hii itakapo kabidhiwa makabrasha ya kufanya kazi watakabidhiwa na hadidu za rejea za kwenda kuangalia wakati wanafanya kazi zao” Amesema Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Tume ya Uchunguzi wa yaliyotokea Octoba 29.





