Kisa Ronaldo, Neves apoteza wafuasi milioni 2 Instagram
Kisa Ronaldo, Neves apoteza wafuasi milioni 2 Instagram
Kiungo wa Ureno na klabu ya PSG, Joao Neves, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kuripotiwa kupoteza zaidi ya wafuasi milioni mbili kwenye mtandao wa Instagram kufuatia kauli yake dhidi ya nahodha wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo.
Neves amekuwa gumzo mitandaoni tangu baada ya sare ya 1-1 iliyoipata Ureno dhidi ya DR Congo katika mchezo wa kwanza wa kundi K la michuano ya Kombe la Dunia 2026, ambapo alidaiwa kueleza kuwa Ronaldo ni mchezaji wa kawaida kama wengine.
Kauli hiyo iliwakasirisha baadhi ya mashabiki wa Ronaldo duniani ambao waamini kwamba nahodha huyo hakupewa heshima anayostahili kutokana na mafanikio yake makubwa katika soka duniani.
Mara baada ya mahojiano hayo kusambaa, akaunti za Neves kwenye mitandao ya kijamii zilianza kushambuliwa kwa maoni mazito kutoka kwa mashabiki wa Ronaldo, huku ripoti mbalimbali za mtandaoni zikidai kuwa kiungo huyo alipoteza zaidi ya wafuasi milioni mbili ndani ya muda mfupi.
Inadaiwa kabla ya mechi hiyo Neves alikuwa na wafuasi milioni tano, lakini baada ya kumzungumzia Ronaldo walipungua hadi hii leo, Juni 20, 2026 kubakia milioni tatu.





