Ligi Kuu NBC hadi mwisho wa msimu nitawashangaa Kamati ya Tuzo kumnyima tuzo ya beki bora 2023/24.

NITASHANGAA KAMA KAMATI YA TUZO ITAMNYIMA TUZO IBRAHIM BACCA 🥇

IMEANDIKWA NA maregesnyamaka

Nimefuatilia mabeki wengi sana wa kati zikiwamo timu tatu za juu Ligi Kuu NBC, Yanga, Azam na Simba. Azam imekua ikifanya rotation, kuna wakati unamuona Edward Manyama, Daniel Amoah, Yannick Bangala na Mcolombia. Wote wanafanya kazi nzuri.

Simba inao Henock Inonga na Che Malone. Daraja lao linafahamika, ni mabeki wakubwa, lakini kwa siku za karibuni kuna makosa wanayafanya yanayojirudia mara kwa mara hasa kwenye clearance kidogo wemekuwa na timing mbovu. Kuna shida ya mawasiliano.

Yanga inawatumia zaidi Dickson Job na Ibrahim Bacca. Wanapiga sana mzigo. Katika orodha yote hiyo ya mabeki wa kati, ni Bacca ambaye amekuwa na ufanisi mkubwa.

Ndiye ambaye ana wastani mzuri wa kufanya tackling ndani ya 18, ndani ya sita. Ndiye anayeongoza kwa kufanya clearance. Mfano mechi kubwa Africa nzima inafuatilia, Yanga dhidi ya Mamelodi pale Lupaso alifanya clearance hatarishi sita, mchezo wa marudiano akiondosha hiyo mipira hatarishi kwenye box mara nane.

Akiwa na muendelezo huu Ligi Kuu NBC hadi mwisho wa msimu nitawashangaa Kamati ya Tuzo kumnyima tuzo ya beki bora 2023/24.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button