Maandalizi ya Chan na Afcon
Mwenyekiti wa Kikao cha kamati ya maandalizi ya mashindano ya CHAN 2024 na AFCON 2027 (LOC) Leodigar Tenga leo tarehe 14 Juni 2025 ameongoza kikao kilichofanyika katika hotel ya Four Points by Sheraton Jijini Dar es salaam.
Lengo la kikao lilikuwa kupokea taarifa ya ukaguzi wa viongozi wa CAF uliofanyika tarehe 25 hadi 28 Mei 2025 pamoja na kupokea taarifa ya kamati ndogo za LOC ya hatua iliyofikiwa katika maandalizi kuelekea mashindano hayo.






