Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango na mwenza wake, Mbonimpaye Mpango leo Machi 31, 2024 wameungana na waumini mbalimbali kushiriki ibada ya Sikukuu ya Pasaka

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango na mwenza wake, Mbonimpaye Mpango leo Machi 31, 2024 wameungana na waumini mbalimbali kushiriki ibada ya Sikukuu ya Pasaka katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Damu Azizi ya Yesu – Kisasa Mkoani Dodoma.

Akitoa salamu za Sikukuu ya Pasaka, Dkt. Mpango ametoa wito kwa watanzania kutumia sikukuu hiyo kutambua kuwa hakuna ushindi bila kujitoa muhanga kwaajili ya wengine, familia, wahitaji na Taifa kwa ujumla.

Amesema ni lazima kujitoa muhanga kwa kutimiza wajibu vizuri… kwa kufanya kazi kwa bidii kwaajili ya maendeleo ya sasa na vizazi vijavyo.

Dkt. Mpango amesema ni muhimu kutumia sikukuu hiyo kujifunza kushinda ubinafsi na kuhakikisha haki na huduma zinatolewa bila kuomba rushwa.

Pia ametoa wito kwa viongozi na watumishi wa serikali kuwa kielelezo cha kujitoa muhanga kwaajili ya kuwatumikia watu wengine. Amesema watanzania wanapaswa kuendelea kumcha Mungu pamoja na kutunza urithi wa dunia uliyotolewa na Mwenyezi Mungu ikiwemo mazingira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button