Mchezaji El Ghazi Avunjiwa mkataba kisa Palestine

Klabu ya Mainz imetangaza kusitisha mkataba na nyota WA soka kutoka Misri Anwar El Ghazi baada ya nyota huyo kuendelea kuiunga mkono Palestina kupitia mitandao ya kijamii.

Nyota huyo amekuwa akipinga mauaji yanayofanywa na majeshi ya Israel kwa Palestina kupitia mitandao yake yake ya kijamii

Baada ya Mainz kutangaza kusitisha mkataba na nyota huyo, El Ghazi kupitia ukurasa wake wa Instagram alijibu kwa kuandika.

“Simamia kilicho sawa hata ikiwa inamaanisha kusimama peke yako

Upotevu wa riziki yangu si kitu ukilinganisha na jehanamu inayoachiliwa kwa wasio na hatia, walio hatarini huko Gaza. Acheni mauaji”.

El Ghazi amevunjiwa mkataba baada ya kuendelea Kuiunga mkono Palestina licha ya Klabu ya Mainz kuisimamisha.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button