Mhe. Dkt. Doto Biteko akisalimiana na Waziri wa Ujenzi, innocentbash pamoja na viongozi wengine
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akisalimiana na Waziri wa Ujenzi, innocentbash pamoja na viongozi wengine wakati alipowasili katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Arusha (AICC) katika Ufunguzi wa Kongamano la Wiki ya Mipango kwa mwaka 2023, leo tarehe 27 Novemba 2023.
Kongamano hilo lina lengo la kuweka msisitizo katika kuimarisha dhana ya kupanga pamoja miongoni mwa wadau wa mipango ya mandeleo nchini.
Kauli mbiu ya Kongamano hilo ni, “Fikra za Pamoja na Utekelezaji ulioratibiwa kwa Ustawi Jumuishi” (Connected Thinking and Coordinated Execution for Inclusive Prosperity).







