Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesisitiza kuwa Watanzania wana wajibu wa kulinda Muungano, amani, utulivu na umoja wa kitaifa wakati wote.
Gombani, Pemba | 02 Aprili 2026
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesisitiza kuwa Watanzania wana wajibu wa kulinda Muungano, amani, utulivu na umoja wa kitaifa wakati wote.
Akizindua Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, amesema Mwenge huo unaendelea kuhamasisha uwajibikaji na mapambano dhidi ya umasikini, ujinga na maradhi kwa kuendeleza maono ya viongozi waasisi wa Taifa.
Rais Dkt. Mwinyi ameonya dhidi ya ubaguzi kwa kusisitiza kuwa huleta migawanyiko na machafuko, huku akihimiza umoja, uzalendo na mshikamano wa kitaifa.
Pia amevitaka vyama vya siasa kutanguliza maslahi ya Taifa na kulinda tunu ya amani, na kuwataka wananchi kushirikiana na Serikali kupambana na rushwa.
Kwa upande wa afya, amesema juhudi zinaendelea katika kupambana na UKIMWI, dawa za kulevya na malaria, ambapo hatua kubwa zimefikiwa katika tiba, kinga na udhibiti wa magonjwa.
Mwenge wa Uhuru umeanza rasmi mbio zake Chakechake, Kusini Pemba, ukiwa na kaulimbiu: “TANZANIA NI YETU SOTE, TUSHIKAMANE.” 🇹🇿






