Mhe. Jerry Silaa amewataka watumishi wa sekta ya ardhi nchini kuiboresha sekta ya ardhi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amewataka watumishi wa sekta ya ardhi nchini kuwa tayari kwa mabadiliko yenye lengo la kuiboresha sekta ya ardhi.
Silaa amesema hayo leo tarehe 21 Septemba 2023 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na watumishi wa sekta ya ardhi katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ikiwa ni mara yake ya kwanza kukutana na watumishi hao tangu ateulie kuwa waziri wa wizara hiyo.





