Miss Tanzania 2023 Ajiondoa Kushiriki Mashindano ya Miss World.

Miss Tanzania 2023 Ajiondoa Kushiriki Mashindano Ya Miss World

Miss Tanzania 2023, Tracy Nabukeera ametangaza rasmi kutoshiriki kwenye mashindano ya Miss World 2025. Kupitia taarifa aliyochapisha kwenye Instagram.

Tracy amesema uamuzi huo haukuwa rahisi, lakini umechukuliwa kutokana na ukosefu wa msaada mawasiliano duni, na maandalizi yasiyoridhisha kutoka kwa waandaaji waliopaswa kumwezesha kuiwakilisha Tanzania kimataifa.

Tracy amesema hakujihisi tena kuwa na nguvu wala kuwa na mazingira ya kumwezesha kusimama kwa ujasiri jukwaani kama mwakilishi wa taifa lake.

Ametoa heshima kwa nafasi aliyopewa kama Miss Tanzania, akisisitiza kuwa mtu anayebeba taji la kitaifa anastahili kupewa msaada wa kutosha na maandalizi bora ili aweze kufanikisha majukumu yake.

Pamoja na kutoshiriki Miss World, Tracy ameahidi kuendelea kutumia taji la #Miss Tanzania-2023kuleta mabadiliko chanya kwa jamii kupitia mradi wake wa Step by Step.

Amehitimisha kwa kutoa shukrani kwa wote waliomuunga mkono katika safari yake hadi sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button