Msanii kutoka Colombia, Shakira, ameweka rekodi mpya kupitia “Las Mujeres Ya No Lloran World Tour” baada ya kufanikisha kuuza jumla ya tiketi milioni moja nchini Mexico pekee.
Msanii kutoka Colombia, Shakira, ameweka rekodi mpya kupitia “Las Mujeres Ya No Lloran World Tour” baada ya kufanikisha kuuza jumla ya tiketi milioni moja nchini Mexico pekee.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kampuni ya OCESA iliyoandaa tour hiyo, idadi hiyo kubwa ya tiketi imeuzwa katika taifa lenye watu takribani milioni 129, ikiwa ni matokeo ya matamasha 26 aliyopanga kuyafanya nchini humo.
Tour hiyo ilianza mwezi Februari 2025 na inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu, huku mafanikio haya yakithibitisha kuwa Shakira bado ni mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa duniani, hususan katika ukanda wa Amerika ya Kusini.
Rekodi hii inaonesha jinsi muziki wake unavyoendelea kugusa nyoyo za mashabiki kwa kiwango kikubwa licha ya kuwa amedumu kwenye muziki kwa miongo kadhaa.