Ni Thomas Muller, Mjerumani asilia na katili kwenye football
Ameshiriki kwenye vichapo vingi vikubwa ambavyo timu yake imevitoa kwa wapinzani (iwe klabuni Bayern Munich au timu ya taifa ya Ujerumani). Kumbuka ushindi wao wa goli 4-0 dhidi ya Ureno kule Brazil mwaka 2014, au ushindi wao maarufu sana wa goli 7-1 dhidi ya mwenyeji Brazil kwenye kombe la dunia mwaka 2014. Magoli yote Thomas Muller anashangilia kwa vibe na energy ileile kama ndo goli la kwanza vile.
Huku Bayern Munich ndio usiseme kwani balaa lake sio la nchi hii. Ameshiriki kwenye zile tano bila nje na ndani alizopigwa Arsenal, zile saba alizochapwa Spurs. Alishangilia kila goli kwenye ushindi wa goli 8-2 dhidi ya Barcelona. Yaani hapoi ila anaboa. Anashangilia kila goli kwa energy ileile.
Ni Thomas Muller, Mjerumani asilia na katili kwenye football








