“Niwakati Wa Mama Kuwatumikia Wananchi Wake” Wema Sepetu

"Niwakati Wa Mama Kuwatumikia Wananchi Wake" Wema Sepetu

“Ni wakati wa Mama kuanza kuwatumikia wananchi wake… Tutanufaika vp na Mema aliotuandalia sisi kama wananchi tuliomchagua kwa Moyo mmoja kama hatutompa nafasi… Ebu tutulieni na tumpe ushirikiano pia katika kujenga taifa…

Kidole kimoja hakivunji chawa… Umoja ni Nguvu… Na ndo tunayohitaji… Mengine tunamuachia Mungu…

Narudia tena, Hakuna haja ya Kuvuruga nchi… Hamsikii… Haiya… Ila tu nasikitika kuona watanzania wanakuwa Misled…

Hili nalo litapita kama yalivyopita mengine….

• But this is just sad… Siwezi kuacha kusimamia na kutetea kile nachoamini sababu ya maneno ya watu… Kila mtu ana haki ya kufanya hivyo… Maneno yenu hayaniuwi, yananikomaza maana Hamjaanza leo, juzi wala jana… And nothing has changed… Naendelea kuwa Sugu… Hakuna jipya ila kwenye ukweli tuambizane tu ukweli… Whats done is done…

Tungetulia tusubirie na tuone matendo na Kazi inayoenda kufanyika… “Wema wa mama” nitaendelea kuwa hapa kuwaleteeni “sio Kwa maneno, bali kwa vitendo” Mema ya Mama yetu… Namba moja wetu… Amri Jeshi mkuu… Si mnakumbuka miradi ni mingi ambayo haijakamilika na mengine mengi yanayotakiwa yafanyike…

Tukaeni kwa Kutulia… Nchi ya Amani hii, Fujo za nini…???”- Ujumbe Kutoka Kwa Wema Sepetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button