Nyuki Wachelewesha Ndege Kupaa kwa Saa 1 India
Nyuki Wachelewesha Ndege Kupaa kwa Saa 1 India.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Ndege ya shirika la IndiGo nchini India imelazimika kuchelewa kwa muda wa lisaa limoja na zaidi baada ya kundi kubwa la nyuki kukaa kwenye mlango wa mizigo wa ndege hiyo.
Ndege hiyo ya Airbus A320 ambayo ilikuwa ikitoka katika mji wa Surat kuelekea Jaipur ililazimika kuondoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Surat saa 11:26 jioni badala ya Saa 10:20 jioni ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa imeeleza kuwa abiria wote walikuwa wameshaingia kwenye ndege pamoja na mizigo yao na ndipo kundi kubwa likavamia na kukaa kwenye mlango huo.
Aidha msemaji wa shirika la ndege la IndiGo ameviamba vyombo vya habari vya India kuwa “Ndege nambari 6E-784
Surat-Jaipur ilichelewa kutokana na tukio la nyuki, ambalo haliko chini ya udhibiti wetu, kwa hivyo safari ya ndege iliondolewa baada ya kibali. Itifaki za kawaida zilifuatwa.”

Hata Hali hiyo imezua taharuki sababisha hali ya taharuki huku wafanyikazi wa uwanja wa ndege wakishangaa jinsi ya ambavyo wangeweza kuwatoa nyuki hao ambapo awali moshi ulitumiwa kuwatawanya nyuki hao na kushindikana huku idara ya zimamoto ikitahadharishwa huku gari la maji la zimamoto likifika eneo hilo na kunyunyiza maji kwenye mlango huo na hatimae nyiki hao kuondoka na kisha ndege kuendelea na safari.





