P Diddy Alimbaka na Kumshambulia Msaidizi Wake wa Zamani, Mahakama Yaeleze.
P Diddy Alimbaka na Kumshambulia Msaidizi Wake wa Zamani, Mahakama Yaeleza.
Aliyekuwa msaidizi wa msanii maarufu wa rapu Sean “Diddy” Combs ameiambia mahakama ya New York kwamba alinyanyaswa na Diddy kingono mara kwa mara alipokuwa ameajiriwa naye kwa miaka minane.
Shahidi huyo – ambaye alitoa ushahidi wake bila kutambulika kwa kutumia jina bandia la “Mia” – pia alisema huku akibubujikwa na machozi kuwa aliishi kwa hofu kubwa alipokuwa akifanya kazi kwa Bw Combs.
Mwanamuziki huyo alitazama akiwa upande wa mshtakiwa huku mikono yake ikiwa imekunjwa mapajani wakati shahidi huyo anaelezea juu ya hofu yake ya kudhurika ikiwa angeripoti madai ya unyanyasaji aliokuwa anapitia.
Bw Combs, 55, amekanusha mashtaka aliyofunguliwa na serikali ya kupanga njama, kutekeleza ulanguzi wa ngono, na usafirishaji ili kujihusisha na ukahaba.
Onyo: Simulizi hii ina maelezo ambayo baadhi ya wasomaji wanaweza kuona ya kuhuzunisha
“Singeweza kumkatalia,..” alisema. “Sikuweza kumwambia hapana kwa lolote.”
Timu ya wanasheria ya Bw Combs bado haijapata nafasi ya kumhoji Mia, au kujibu madai yake.
Yeye ni shahidi wa pili katika kesi hiyo kudai kuwa Bw Combs alimnyanyasa kingono, pamoja na mpenzi wa zamani wa Bw Combs, Casandra Ventura.





