Raia wa Nigeria Wakamatwa Kenya Wakifanya Utapeli

Raia wa Nigeria Wakamatwa Kenya Wakifanya Utapeli.

Polisi nchini Kenya wamewakamata raia watatu wa Nigeria wanaodaiwa kuishi nchini humo kinyume na sheria na kujihusisha na uhalifu ikiwemo utapeli mtandaoni.

Walikamatwa tarehe 12 Novemba 2025 katika kijiji cha Mwihoko, Ngurubani, Mwea East baada ya oparesheni ya pamoja ya polisi na maafisa wa uhamiaji kufuatia taarifa kutoka kwa wananchi.

Vifaa vilivyopatikana ni pamoja na simu 21, laini 79, kompyuta mpakato, kadi 37 za benki mbalimbali, fedha za nchi saba na unga mweupe pamoja na vifaa vinavyoshukiwa kutumika kwa uchawi. Uchunguzi umebaini kuwa watatu hao walifika Kenya kati ya 2021 na Januari 2025 na wamekiuka masharti ya viza zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button