RAIS DANIEL CHAPO AWASILI ZANZIBAR KWA ZIARA YA KIKAZI

Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe @daniel_chapo24 tayari amewasili Zanzibar akitokea Jijini Dar es Salaam ambapo akiwa Zanzibar atakua na ziara fupi ya kikazi.

Akiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume amepokelewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Hamza Hassan Juma, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. @mahmoudkombo (Mb.), Mhe. @angellah_kairuki (Mb.), Mshauri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na viongozi wengine wa serikali.

Rais Chapo atakutana na Mwenyeji wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt @DrHmwinyi pamoja na kutembelea kituo cha Uvuvi cha Bahari kuu Fumba.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button