Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi amefariki

Rais wa zamani wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi, amefariki dunia leo Februari 29, 2024 akiwa na umri wa miaka 98.

Taarifa hizo zimetangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania. Rais Samia amesema, Mwinyi ameaga dunia wakati akipatiwa matibabu ya saratani ya mapafu kwenye hospitali moja ya serikali mjini Dar es Salaam.

Mwinyi –aliyefahamika na wengi nchini Tanzania kwa jina la “Mzee wa ruksa“ kutokana na sera zake za mageuzi ya kiuchumi ya kiliberali na soko huria– anaacha historia ya kuwa mwanasiasa pekee hadi sasa aliyeshika wadhifa wa rais wa Tanzania pamoja na Zanzibar, visiwa vyenye mamlaka yake ya ndani ambavyo ni sehemu ya taifa hilo la Afrika Mashariki.

Rais Samia ametangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa na bendera zote za nchi hiyo zitapepea nusu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button