Rais Samia ashiriki misa ya kumwombea Kardinali Pengo
Rais Samia ashiriki misa ya kumwombea Kardinali Pengo
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ni miongoni mwa viongozi mbalimbali wanaoshiriki misa ya kumwombea marehemu Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo katika Kanisa Kuu la Mt. Joseph jijini Dar es Salaam.
Kardinali Pengo (82) alifariki dunia Februari 19, 2026 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya moyo.
Misa ya kumwombea imeanza kanisani hapo Saa 10:00 jioni leo ljumaa, Februari 27, 2026 ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo maaskofu, watawa wa kiume na kike dini, Serikali, vyama vya siasa na waumini wa Kanisa Katoliki Mbali na Rais Samia, wengine waliopo ni Makamu wa Rais, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba, Spika wa Bunge, Mussa Zungu na mawaziri mbal;imbali.
Mwili wa Kardinali Pengo utazikwa kesho Jumamosi, katika Kituo cha Hija Pugu jijini Dar es Salaam alipochagua mwenyewe.





