Rais Samia Asisitiza Maadili Katika Kuwajenga Kujiamini.
Rais Samia Asisitiza Maadili Katika Kuwajenga Watoto Kujiamini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kujenga kizazi chenye maadili mema na chenye kuheshimiana ili kuwa jamii bora itakayozaa Taifa imara.
Wakati wa hotuba yake kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani leo Machi 08, 2025 Jijini Arusha, Rais
Samia pia amesisitiza umuhimu wa kulea watoto wanaojiamini na wenye uwez0 wa kujenga hoja badala ya kuwa na vijana wasiojiamini na wenye kupaza sauti bila
ya kuwa na hoja zenye kueleweka.
Rais Samia pia amesisitiza Vijana kujitambua akisema hayo ndiyo mambo pekee ambayo yanaweza kufanikisha
malengo na ndoto za Tanzania za kuwa na Taifa jumuishi lenye ustawi na haki ambalo litakwenda kinyume na ubaguzi mbalimbali katika ngazi ya Jamii.
Rais Samia pia amesisitiza umuhimu wa kuwa na serikali inayoamini katika usawa wa Kijinsia, akiwataka wanawake na Sekta mbalimbali kuhamasisha jamii kujiandikiaha kwenye daftari la Mpigakura ili kuendelea
kusimamia usawa wa kijinsia kwakuwa na serikali inayoamini katika usawa pamoja na kudumisha utulivu, amani na kukuza demokrasia.








