Sanamu Isiyo Onekana Yauzwa Kwa Shilingi Milioni 44.

Sanamu Isiyo Onekana Yauzwa Kwa Shilingi Milioni 44.

Mei 2021, msanii wa Kiitaliano Salvatore Garau aliifanya dunia kushangaa baada ya kuuza sanamu isiyokuwepo kabisa, iliyopewa jina “lo Sono” (Mimi Nipo), kwenye mnada wa Art-Rite huko Milan. Kilichouzwa sio kitu cha kushika, ni nafasi tupu ya futi 5 kwa 5 pamoja na cheti cha uthibitisho kinachoeleza mahali pa kuisimamisha “sanamu”.

Kazi hiyo ilinunuliwa kwa zaidi ya shilingi milioni 44, lakini cha kushangaza zaidi ni kwamba mnunuzi hakujulikana. Ripoti zinasema ilikuwa ni mtu binafsi, mtu aliyetamani kuwa sehemu ya mjadala mpana wa “sanaa ya kufikirika”.

Kwa nini mtu alinunua kitu kisichoonekana?

Kwa mujibu wa Garau, “lo Sono” imeundwa kwa “hewa na roho”, ikiashiria uwepo ambao hauhitaji macho bali fikra. Ni kazi inayolenga kutikisa tafsiri ya watu kuhusu uwepo, nguvu ya mawazo, na thamani ya kile tusichokiona.

Hivyo, mnunuzi hakulipa kwa ajili ya kitu cha kuweka sebule… alilipa kwa wazo, falsafa, na hadhi ya kuwa sehemu ya historia ya sanaa ya kisasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button