Simba sc Wamfuata Jocye Lomalisa
Wakati Tetesi za usajili zikimhusisha beki wa Yanga, Joyce Lomalisa kujiunga na Simba mwenyewe kaibuka na kuweka wazi kuwa yupo tayari kucheza timu yoyote Tanzania Bara lakini kwa masharti.
Lomalisa ambaye ni raia wa DR Congo aliyesalia kwenye kikosi cha Yanga, anamaliza mkataba wake na mwishoni mwa msimu huu baada ya kuitumikia kwa misimu miwili akitwaa mataji ya ndani na kucheza hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika, Lomalisa ambaye anakubalika kwa kumwaga majalo, alikiri kuwa bado ni mchezaji wa Yanga kwa mujibu wa mkataba ambao ameweka wazi kuwa unamalizika mwisho wa msimu huu.
🎙️Mimi bado ni mchezaji wa Yanga watu ndio wanaandika wanachojisikia mwisho wa msimu kila kitu kitajulikana kwasababu ndio mkataba unamalizika hivyo kama ntabaki au ntaondoka kila mmoja atafahamu.” Alisema na kuongeza
🎙️Napenda kubaki Yanga lakini hawajanifuata kwaajili ya mazungumzo ya mkataba mpya nimebakiza mwezi mmoja tu hakuna mazungumzo yoyote hivyo kama kuna timu zinahitaji huduma yangu zinatakiwa kuwasiliana na meneja wangu yupo Angola.”
“Mchezaji unaenda kwenye timu ambayo una uhakika wa kupata maisha mazuri na kutumikia mkataba wako kwa usahihi kuanzia kucheza na kuipa timu matokeo hivyo ili nitoke hapa natakiwa kuzingatia hivyo vitu.”
Akizungumzia hali ya afya yake na Moja ya Chanzo chetu baada ya kuumia kwenye mchezo dhidi ya Singida Fountaine Gate Yanga wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0, alisema Joyce anaendelea vizuri na ameanza mazoezi ya gym.
“Naendelea vizuri,ninaanza mazoezi hivyo naamini mechi inayofuata naweza kupata nafasi ya kurudi kucheza.”
“Nikiwa fiti nina uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza hiki ndio nakitaka ikitokea nikapata nafasi ya kuondoka Yanga timu ambayo bado natamani kuendelea kuitumikia lakini sioni nafasi kutokana na viongozi kutokufanya mazungumzo na mimi hadi muda huu.”
Alisema mlinzi huyo wa kushoto raia wa Congo DR
JUA NI NGUMU MCHEZAJI KUONDOKA IKIWA KIKOSINI YANGA WAKIWA BADO WANA MAHITAJI NAWEWE ZAIDI (Imefahamika hivyo).







