Sishikiki na Mapenzi yake kwa Ibrahim Traore.

Sishikiki na Mapenzi yake kwa Ibrahim Traore.

Mwanamitindo na mhamasishaji wa mitandaoni, Sishkiki, amezua gumzo mitandaoni baada ya kuelezea wazi mapenzi yake kwa lbrahim Traoré, kiongozi kijeshi wa Burkina Faso.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sishkiki alimuelezea Traoré kama “African Giant”, “Simba la Masimba”, na “the real OBO of Africa”, akisisitiza kuwa ni kiongozi
anayewafanya Waafrika wote kusimama na kumpa heshima kubwa.

Sishkiki alisema licha ya Traoré kuwa na umri wa miaka 37, ana busara na akili za mtu mzima, na hajawahi kufikiri kuwa angeweza kumpenda mwanaume mwenye umri
mdogo kama huo.

“Nadhani nimeanguka kimapenzi,
aliandika. Katika ujumbe wake wa kihisia, alimalizia kwa kusema: “Kufuta deni lote la nchi ndani ya awamu moja si mchezo,”
akionyesha kuvutiwa pia na uwezo wa Traoré wa kusimamia nchi na kuchukua maamuzi magumu kwa ajili ya watu wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button