Tani 61,000 za Mbolea NPK zawasili mkoani mbeya kabla ya msimu wa nvuwa

Jumla ya tani 61,000 za mbolea ya NPK (Nitrogen, phosphate na potash 10:18:24) zimewasili nchini tarehe 17 Septemba, 2024 na kukabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe .Juma Homera kwa ajili ya shughuli za kilimo katika mkoa huo.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) amesema makabidhiano hayo yatasaidia katika kuhakikisha kunakuwa na usalama wa mbolea nchini na kuhakikisha mbolea hiyo inawafikia wakulima, vyama vya ushirika, wafanyabiashara pamoja na wasambazaji wa mbolea nchini kwa wakati.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mbolea Tanzania, Bw. Samuel Mshote amesema kuwa mbolea hiyo ni kati ya tani 130,000 zinazotarajiwa kuingia nchini kufuatia maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha mbolea za mazao yote nchini zinawasili kabla ya kuanza kwa msimu wa kilimo.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amesema Serikali itahakikisha mbolea hiyo inawafikia wakulima wote waliopo mijini na vijijini katika kuhakikisha mkulima wa tumbaku anazalisha kwa tija zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button