Taraja Ramsess, mwigizaji na msanii wa karate kwenye filamu za “Black Panther” na “Avengers”, amefariki dunia pamoja na watoto wake watatu
Taraja Ramsess, mwigizaji na msanii wa karate anayejulikana kwa kazi yake kwenye filamu za “Black Panther” na “Avengers”, amefariki dunia pamoja na watoto wake watatu kutokana na ajali ya gari huko Georgia wiki iliyopita. Kituo cha Televisheni cha Atlanta WSB-TV kiliripoti kwamba, ajali hiyo ilitokea kabla ya saa sita usiku siku ya Halloween baada ya gari waliokuwa wakisafiria kugongana na trela ya trekta ambayo ilikuwa imeharibika katika njia upande wa kushoto mwa barabara.
“Mwanangu mtanashati, mpendwa na mwenye talanta Taraja chop.saki, pamoja na wajukuu zangu wawili, binti yake wa miaka 13 Sundari na binti yake mchanga Fujibo mwenye umri wa wiki 8, waliuawa usiku uliopita katika ajali mbaya ya barabarani,” aliandika Mama yake mzazi, Bi. Akili Ramsess.
Pia aliandika kwamba mabinti wawili wa Ramsess walinusurika kwenye ajali hiyo, na mtoto wake wa miaka mitatu, Shazia, amelazwa hospitalini na mtoto wake wa kiume wa miaka 10, Kisasi, ambaye aliandika kwamba alikuwa kwenye chumba cha dharura lakini kwa taarifa mpya ni kwamba Kisasi naye amefariki dunia.









