Timu Ya Iran Yakwepa Kuimba Nyimbo Ya Taifa.

Timu Ya Iran Yakwepa Kuimba Nyimbo Ya Taifa.

Wachezaji wa Timu ya Wanawake ya mpira wa miguu ya Iran wamezua gumzo mitandaoni baada ya kukwepa kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa Kombe la Asia la Wanawake 2026 Nchini Australia na badala yake Wachezaji hao walikaa kimya wakati wimbo huo ukipigwa uwanjani.

Kitendo hicho kimetafsiriwa na wengi kama ishara ya msimamo wao katika kipindi ambacho Nchi yao inapitia mvutano mkubwa wa kisiasa na kijeshi katika eneo la Mashariki ya Kati ambapo baadhi ya Wachambuzi wamesema kitendo hicho kinaweza kuwa ishara ya ujumbe wa kisiasa au mshikamano na Raia wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali ndani ya Nchi yao.

Hata hivyo hakuna tamko rasmi kutoka kwa Wachezaji au Viongozi wa Timu hiyo kuelezea sababu kamili ya uamuzi huo wa kukataa kuimba wimbo wa Taifa lao ambapo katika mchezo huo wa ufunguzi wa mashindano, Iran ilipoteza kwa kufungwa 3-0 dhidi ya Korea Kusini lakini tukio la kukataa kuimba wimbo wa Taifa ndilo lililovuta zaidi mijadala kwenye mitandao ya kijamii na Vyombo vya Habari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button