Trump Adhibitisha Jeshi la Marekani Limeshambulia Iran
Trump Adhibitisha Jeshi la Marekani Limeishambulia Iran
Rais Donald Trump wa Marekani, ametangaza kuwa Vikosi vya Jeshi la Marekani vimerusha mabomu kwenye vituo vitatu vya nyuklia vya Iran na hivyo kuhitimisha kipindi cha wiki moja cha mashauriano kuhusu kujiunga na kampeni ya Israel dhidi ya Iran na kuiingiza Marekani moja kwa moja katika mzozo huo unaozidi kushika kasi.
Katika andiko lake hilo, Trump amesema Ndege zote za Jeshi la Marekani zilizohusika katika mashambulizi hayo ya Iran tayari zimeshaondoka ndani ya anga la Iran.

“Tumekamilisha mashambulizi yetu yenye mafanikio makubwa kwenye maeneo matatu ya nyuklia Nchini Iran ikiwa ni pamoja na Fordow, Natanz na Esfahan, Ndege zote sasa ziko nje ya anga ya Iran” Trump aliandika kwenye Mtandao wake wa Kijamii wa Social Truth.
Katika andiko hilo la Trump aliongeza kwa kusema “hakuna Jeshi jingine duniani ambalo lingeweza kufanya hivi, SASA NI WAKATI WA AMANI” #MillardAyoUPDATES





