Trump Akutana na Biden Ikulu White House.

Trump Akutana na Biden Ikulu White House.

Donald Trump alirejea Washington na
kutembelea Ikulu ya White House kwa mkutano na Rais Joe Biden katika Ofisi ya Oval. Trump ameahidi kubadilishana mamlaka huku akiendelea kujenga utawala
wake mpya kama rais mteule wa Marekani kupitia chama cha Republican.

Biden amempongeza Trump kwa ushindi katika uchaguzi wa Novemba 5, akimtakia mafanikio na kuahidi “mabadiliko laini.”

Trump amekubali ahadi hiyo na kumshukuru Biden kwa mwaliko, jambo ambalo yeye alikataa kutoa kwa Biden baada ya kushindwa uchaguzi wa 2020.

Trump pia alisusia sherehe za uapisho wa Biden zilizofanyika Januari 2021. Trump amesema, “Siasa ni ngumu, lakini leo ni
ulimwengu mzuri na tunaweza kuthamini mabadiliko haya.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button