Umaarufu Wapunguza Siku za Kuishi za Mwanamziki
Umaarufu Wapunguza Siku za Kuishi za Mwanamziki.
Utafiti wa Chuo Kikuu cha Witten Herdecke nchini Ujerumani umebaini kuwa umaarufu unaweza kupunguza maisha ya wanamuziki kwa wastani wa miaka 4.6.
Kwa kuchambua taarifa za waimbaji 648, watafiti waligundua kuwa wanamuziki mashuhuri walifikia wastani wa miaka 75, huku wale wasio maarufu sana wakiishi hadi miaka 79.
Vyanzo vya kupungua kwa maisha vinatajwa kuwa ni pamoja na kupoteza faragha, shinikizo la kazi na changamoto nyingine zinazohusiana na umaarufu.





