“Vijana Msikate Tawi Mlilokalia” Samia

"Vijana Msikate Tawi Mlilokalia" Samia

“Pamoja na kuwa uchaguzi ulifanyika, kulijitokeza vurugu za uvunjifu wa amani ambao ulisababisha uharibifu wa mali, kupoteza maisha na kuhatarisha usalama wa Nchi, tunapoenda mbele niwasihi sana Watanzania tuongozwe na dhamira ya maelewano, ushirikishwaji, kujirekebisha na umoja”

“Kwa Wanangu Vijana wa Taifa hili la Tanzania niseme kwamba nchi hii imejengwa kwenye misingi ya amani na utulivu wakisiasa, sisi Wazazi wenu kama tungeyafanya mliyoyafanya wakati huu Nchi hii isingekuwa na neema na maendeleo mnayoyaona leo”

“Narudia hilo, kwa Wanangu Vijana wa Tanzania, sisi Wazazi wenu kama tungeyafanya mliyoyafanya nchi hii isingekuwa na neema na maendeleo mnayoyaona leo, hivyo niwasihi sana Wanangu Vijana wa Taifa hili, nchi hii ni yenu kwa shida zozote zile zinazowakabili, msikubali hata siku moja kushawishishiwa kuichoma nchi yenu wenyewe”

“Msikubali kukata tawi la nchi mliyoikalia msikubali kabisa, hili nawaomba mlikate kwa nguvu zenu zote, nyie ndio Wajenzi wa Taifa hili nawasihi kamwe msiwe Wabomoaji wa Taifa hili” — Rais Samia akihutubia Bunge leo November 14,2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button