Waandishi wa Habari walio uwawa huko Gaza
Picha ikiwaonyesha Waandishi wa habari wa Al Jazeera, Anas Al-Sharif na Mohamed Qreiqeh, @mohammed_qraiqea wakiwa kazini mbele ya kamera katika moja ya ripoti zao za moja kwa moja kutoka Gaza. Wakiwa wamevalia kofia za chuma na fulana zenye maandishi “PRESS,” walijitosa mstari wa mbele kuripoti hali halisi ya mapigano kwa dunia, licha ya hatari kubwa waliokuwa wakikabiliana nayo kila siku.
Picha hii ni ushuhuda wa ujasiri na kujitolea kwao katika kutetea haki ya wananchi kujua ukweli.
Leo, dunia inaomboleza vifo vyao, lakini picha kama hii itaendelea kuwa kumbukumbu ya dhamira yao isiyotetereka katika kuandika historia.






