Wachezaji wa Timu Taifa ya Tanzania walienda Umrah

Baadhi ya wachezaji na sehemu ya benchi la ufundi la Timu ya Taifa ya Tanzania (taifastars_), walienda kufanya ibada ya Umrah katika msikiti mtukufu wa Makkah ambao upo nchini Saudi Arabia baada ya kumalizika kwa mechi Kirafiki ya Kimataifa dhidi ya Sudan.

Kutoka mji wa Al Taif ambako mechi ilichezwa hapo jana, Oktoba 15 kwenda mji ambao Msikiti huo unapatikana ni mwendo wa saa moja tu kwa gari.

Katika mchezo huo Taifa Stars ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Sudan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button