Waitwe Mama Lishe Sio Mama Ntilie
Waitwe Mama Lishe Sio Mama Ntilie
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekubaliana na ombi la Umoja wa Mama Lishe na Baba Lishe Tanzania (UMALITA) la kuitwa Baba Lishe na Mama Lishe badala ya kuitwa Mama Ntilie au Baba Ntilie.
Akizungumza leo April 21,2026 Jijini Dar es salaam, wakati wa Kongamano la Kitaifa la Mama Lishe na Baba Lishe, Rais Samia amesema “Shughuli za Mama Lishe na Baba Lishe zinastahili kuthaminiwa na kuheshimiwa kwa hadhi inayolingana na mchango wao wa kila siku, yale yaliyosemwa hapa ya kunyanyaswa, ya kusumbuliwa hayapaswi kufanya kwa kundi hili ni kundi linalotupa uhai, tunawaheshimu na Serikali itasimamia heshima yenu”
“Nakubaliana nanyi kubadilisha jina kutoka Mama Ntilie na Baba Ntilie kwenda Mama Lishe na Baba Lishe na hilo sasa ndio jina rasmi”



