“Nitakuwa Mlezi Wenu Nikimaliza Urais”Samia
"Nitakuwa Mlezi Wenu Nikimaliza Urais" Samia
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema akimaliza kipindi chake cha Urais wa Tanzania, atakuwa Mlezi wa Umoja wa Mama Lishe na Baba Lishe Tanzania (UMALITA) kama umoja huo ulivyomuomba.
Rais Samia amesema hayo leo April 21,2026 wakati akifungua Kongamano la Kitaifa la Mama Lishe na Baba Lishe Jijini Dar es salaam.
Rais Samia amesema “Kuliletwa pia maombi, ombi la kwanza ni Rais kuwa Mlezi wa umoja huu, sasa nikiwa Rais wa Tanzania nakuwa Mlezi wa makundi yote ndani ya Nchi, ila kwa kundi hili nataka niwape faida, nitakapomaliza Urais wa Tanzania na kama nitakuwa hai InshaAllah nitakuwa Mlezi wa kundi hili lakini miaka minne hii penye uhai na uzima basi nisaidiwe hiyo kazi mpaka pale nitakapomaliza kazi hii (kazi ya Urais) basi nitakuwa Mlezi wa kundi hili” amesema Rais Samia





