Wana CCM Tuheshimu Maamuzi ya Vikao.

Wana CCM Tuheshimu Maamuzi ya Vikao.

Aliyekuwa Mbunge wa viti maalum na Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM Munde Tambwe awaomba Wanachama na wapenzi wa chama waheshimu maamuzi ya vikao kwakuwa misingi yao ni maadili na waungane kwa pamoja kuhakikisha ushindi mzito kwa Rais , Wabunge na madiwani

Munde amesema hayo punde baada ya sintofahamu za hapa na pale kwa baadhi ya Wanachama wa Chama hiko kuzua taharuki baada ya mamlaka za juu za chama kutangaza majina yaliyopitishwa kwaajili ya kugombea rasmi kwakuwakilisha Chama katika uchaguzi mkuu 2025 ikiwemo majina ya Wabunge

Amesema

“Nakishukuru Chama changu kwa maamuzi ya uteuzi wa mgombea Jimbo la Sikonge kwa moyo mkujufu niwaombe wanaccm wenzangu tuungane kuhakikisha CCM inashinda kwa kura nyingi nafasi ya Rais, Mbunge na Madiwani Kazi na utu Tunasonga Mbele ” _Munde_

Hata hivyo ameongeza kuwa
Wanaccm wenzake anawaomba waheshimu maamuzi ya Vikao na ndio maadili ya Chama pia amekishukuru Chama kwa heshima iliyompa na kwa moyo mkunjufu amewaomba waungane kutafuta ushindi wa CCM wa Rais, Mbunge na Madiwani

Aidha Ikumbukwe Munde Tambwe ndiye aliibuka mshindi wa kura za maoni jimbo la Sikonge, Mkoani Tabora

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button