Watatu wakamatwa Kifo cha Liam Payne

Watatu wakamatwa Kifo cha Liam Payne

Watu watatu wamekamatwa nchini Argentina wakihusishwa na kifo cha mwanamuziki maarufu wa One Direction, Liam Payne, aliyeaga dunia baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya tatu ya hoteli ya Casa Sur mjini Buenos Aires, Oktoba 16.

Kwa mujibu wa ofisi ya mwendesha mashtaka Andres Esteban Madrea, mtuhumiwa mmoja ameshtakiwa kwa kosa la kumwacha mtu hadi kusababisha kifo na pia kwa kuhusika na usamnbazaji wa dawa za kulevya.

Ofisi hiyo ilieleza kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akifuatana na #LiamPayne kila siku wakati wa ziara yake nchini humo.

Mfanyakazi mmoja wa hoteli na mtu mwingine wa tatu pia wamneshtakiwa kwa kuhusika na usambazaji wa dawa za kulevya.

Mwendesha mashtaka aliondoa uwezekano wa marehemu kujidhuru, akieleza kuwa Liam Payne hakuchukua hatua yoyote kujikinga wakati wa kuanguka, hali inayoashiria alikuwa katika hali ya kupoteza fahamu.

Matokeo ya uchunguzi wa sumu yalionyesha alama za pombe, kokeini, na dawa za kupunguza mawazo mwilini mwa msanii huyo kabla ya kifo chake, na uchunguzi unaendelea kwa uchambuzi zaidi wa vifaa vyake vya kibinafsi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button