WAZIRI KATAMBI ATIA SAINI HATI YA MAKUBALIANO KATIKA MASUALA YA UHAMIAJI KATI YA TANZANIA NA SOMALIA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Patrobas Katambi, amesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Somalia, Jenerali Abdullahi Sheikh Ismail (Fartaag), kuhusu masuala ya kiuhamiaji kati ya nchi hizo mbili.

​Hati hiyo iliyosainiwa leo jijini Dar es Salaam, imelenga kuondoleana hitaji la visa kwa wamiliki wa Pasipoti za kidiplomasia na za kiutumishi, pamoja na kuimarisha mashirikiano katika masuala ya uhamiaji baina ya Tanzania na Somalia.

​Akizungumza baada ya kusaini hati hiyo, Mhe. Katambi ametambua ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo, ikiwemo mashirikiano katika masuala ya usalama wa raia na kuhamisha wafungwa.

​Vilevile, Mhe. Patrobas Katambi ameeleza kuwa Tanzania itaendeleza ushirikiano na nchi zilizopo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, ili kuhakikisha usalama na amani vinatawala katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki.

Kadhalika, tukio hilo limehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ayoub Mohammed Mahomud, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ally Gugu, Wakuu wa Vyombo vya Usalama

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button