Zuio la Kenya Kwa Madaktari Wakigeni.

Zuio la Kenya Kwa Madaktari Wakigeni

Serikali ya Kenya kupitia Wizara ya Afya imetangaza kusitisha utoaji wa vibali vya kazi kwa madaktari wa kigeni wenye vigezo sawa na madaktari wazawa ikisema vibali vitatolewa tu kwa madaktari bingwa wa kigeni wenye ujuzi maalum usiopatikana nchini humo ambapo hatua hiyo imelenga kulinda ajira za Wataalamu wa afya wa ndani ya Nchi.

Uamuzi huo umeibua upinzani, ambapo Chama cha Madaktari kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kimewasilisha kesi mahakamani kikipinga hatua hiyo, kikidai kuwa inakiuka misingi ya ajira na uhuru wa kufanya kazi ndani ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Vilevile hatua ya Kenya imezua mjadala mpana kikanda kuhusu utandawazi wa ajira ndani ya EAC huku baadhi wakiona ni hatua halali ya kulinda maslahi ya Wazawa na wengine wakionya kuwa inaweza kuhatarisha mshikamano na ushirikiano wa kikanda katika sekta ya afya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button