Vigogo Chadema wakutana na ujumbe wa AFLN Dar

Vigogo Chadema wakutana na ujumbe wa AFLN Dar

Jana Jumatatu, Aprili 20, 2026 uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ulikutana na ujumbe wa Mtandao wa Viongozi Wanawake Afrika (AFLN) uliokuwa ukiongozwa na aliyekuwa Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, akiwa ameambatana na aliyekuwa Rais wa Ethiopia, Sahle-Work Zewde.

Ziara ya ujumbe huo nchini Tanzania inalenga kukutana na makundi mbalimbali, ikiwemo vyama vya siasa na asasi za kiraia, kwa lengo la kukusanya na kufuatilia taarifa kuhusu matukio yaliyotokea kabla na baada ya tarehe 29 Oktoba 2025.

Kwa upande wa Chadema, ujumbe uliongozwa na Makamu Mwenyekiti Bara, John Heche, akifuatana na Katibu Mkuu, John Mnyika; Naibu Katibu Mkuu Bara, Amani Golugwa; Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Ali Ibrahimu na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee, Suzan Lyimo.

Katika kikao hicho, Chadema iliwasilisha msimamo wake rasmi kama ulivyoazimiwa na Kamati Kuu ya chama na kueleza kwa kina matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu na vitendo vya ukatili vinavyodaiwa kutokea kabla, wakati na baada ya tarehe 29 Oktoba 2025.

Chadema kimesisitiza umuhimu wa uchunguzi huru na wa haki, uwajibikaji kwa wote waliohusika, pamoja na kulindwa kwa misingi ya demokrasia, haki na utawala wa sheria nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button