Trending
Diamond Afunika Alikiba Pesa za Mirabaha.
https://youtu.be/N_BDf6BGUIY
Usiku wa kuamkia leo Serikali kupitia Chama cha
Hakimiliki Tanzania (COSOTA) wamegawa Mirabaha kwa wasanii wa
muziki hapa nchini.Msanii @diamondplatnumz ameshika nafasi ya kwanza kwa kupata
mgao wa Mirabaha wa TZS Milioni 7.7 akifuatiwa na @officialalikiba aliyevuna TZS Milioni 5 huku @rayvanny naye akikunja kitita cha TZS Milioni 4.9.Mirabaha hiyo inatokana na makusanyo kutoka sehemu mbalimbali ambako kazi za wasanii nchini zimetumika kibiashara.
Wanufaika wengine katika Keki hiyo ni pamoja na Zuchu Milioni 4.7, Mbosso Milioni 4.3, Nandy Milioni 3.5, Harmonize Milioni 3.4, Maua Sama Milioni 2.3, Young Lunya Milioni 1.6.





