Mtwara marekebisho ya miundombinu ya maji yapamba moto

Magari makubwa yenye shehena ya mabomba ya majisafi kwa ajili ya mradi mkubwa wa marekebisho ya miundombinu ya maji Mtwara mjini yamepokelewa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo, wakiwemo wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mtwara Saidi Nyengedi katika kiwanja cha shule ya msingi Lilungu.

Mradi huo unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 19 ambapo katika mapokezi viongozi hao wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya kuimarisha huduma ya Maji Mtwara mjini, sanjari na Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso (Mb) kwa kusimamia vema maelekezo ya Mhe Rais kuhusu kuboresha miundombinu ya maji Mtwara mjini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mtwara (MTUWASA) Mhandisi Rejea Ng’ondya ametoa maelezo kuhusu ujio wa mabomba ya maji ya maboresho ya miundombinu ya maji yanayoendelea amesema dhamira ya Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha wananchi wa Mtwara wanapata huduma ya maji safi na salama na amedhamiria kumaliza kabisa changamoto ya miundombinu chakavu Mtwara mjini na tayari mradi wa ujenzi wa Chujio la kusafisha maji umekamilika na utazinduliwa wiki ijayo katika ziara ya Mhe. Rais mkoani Mtwara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button