Chanzo cha vidonda vya tumbo na tiba yake
FAHAMU KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO
Vidonda vya tumbo ni tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda, hii hutokea ni baada ya kuharibika kwa ukuta wenye ute unaozuia kemikali za kuyeyusha chakula unaoitwa mucus.
Kemikali ambayo ni acid inayozalishwa mwilini kiasili husaidia kuyeyusha chakula na kuua wadudu tumboni, kama ukuta wenye ute ukiharibiwa na kushindwa kufanya kazi, basi kemikali (acid) itaathiri tumbo au utumbo na kuruhusu bakteria kuendelea kusababisha vidonda vya tumbo.
Vidonda vya tumbo vinatibika kirahisi ila vikicheleweshwa bila kutibiwa huweza kusababisha tatizo kubwa. Ni tatizo linalotesa sana na kuwanyima raha watu wengi. Linahitaji umakini na pia husababisha magonjwa mengine kama kansa, amoeba (amiba), homa, kupungua uzito.
AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO
Kuna aina zipatazo mbili za Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers)
- Vidonda vya tumbo kubwa (Gastric ulcers)
Hivi ni vidonda vya tumbo vinavyotokea ndani kwenye tumbo kubwa
Gastric ulcers
- Vidonda vya utumbo mdogo (Duodenal ulcers)
Hivi ni vidonda ambavyo hutokea kwenye utumbo mdogo (hasa juu)
HATUA KUU ZA VIDONDA VYA TUMBO
Kuna hatua nne yenye matukio na dalili mbalimbali kwenye huu ugonjwa, mengine yaweza kuonekana au mgonjwa asiweze kuhisi chochote. Hatua hizo ni;-
🌻 HATUA YA KWANZA
Ni ule uvimbe sugu unaotokea sehem ya ndan ya tumbo.
🌻 HATUA YA PILI
Hapa vijidonda hujitokeza sehemu zenye uvimbe na taratibu vidonda hivyo huongezeka na kua vikubwa, katika hatua hii mgonjwa hupatwa na maumivu makali ya tumbo yanayodumu kwa muda mrefu yakiambatana na kiungulia, tumbo kujaa gesi wakati wote, kukosa hamu ya kula, choo kuwa kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu, hata hvyo Hali hii ya kukosa choo kwa muda mrefu (CHRONIC DYSPEPSIA) yani kushindwa kufanya Kazi kwa mfumo wa mmeng’enyo wa Chakula kutokana na tindikali nyingi inayozalishwa tumboni na kuingia Kwenye mzunguko wa damu hivyo mgonjwa hujisikia uchovu na kizunguzungu cha Mara kwa Mara katika hatua hii tindikali husababisha magonjwa ya ini na Figo kwa kuwa tayari iko katika mfumo mzima wa damu
🌻 HATUA YA TATU
Ni hatua ambayo ni ya hatari kwasababu vidonda vikubwa hupasua mishipa yote midogomidogo ya damu na kusababisha damu kuvia tumboni na kubadilisha rangi ya choo kuwa cyo ya kawaida, pia damu nyingi ikivujia tumboni mgonjwa hutapika na kuharisha damu Hali hii husababisha mgonjwa kuishiwa damu Mara kwa Mara, maumivu makali ya tumbo,hupata Homa, maumivu ya viungo na kukosa hamu ya kula.
🌻 HATUA YA NNE
Katika hatua hii saratani ya utumbo inahusika kwani katika hatua hii vidonda vya tumbo hutengeneza tundu katika tumbo au utumbo mdogo na kusababisha kuoza kwa viungo vya ndani na matokeo yake ni saratani ya utumbo.
DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
✍Kuchoka choka sana bila sababu maalum.
✍Kuumwa mgongo au kiuno.
✍Kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsia.
✍Kizunguzungu
✍Kukosa usingizi
✍Maumivu makali sehemu ya mwili
✍Maumivu ya Kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali.
✍Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali
✍Kichefuchefu
Kiungulia
✍Tumbo kujaa gesi
✍Tumbo kuwaka moto
✍Maumivu makali sehemu kilipo kidonda
✍Kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi
✍Kutapika nyongo
✍Kutapika damu au kuharisha
✍Sehemu za mwili kupata ganzi
✍Kukosa hamu ya kula
✍Kula kupita kiasi
✍Kusahahu sahau na
✍Hasira bila sababu.
✍Kuwa na ugonjwa wa BAWASILI
CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO
Vidonda vya tumbo vina vyanzo tofauti vyote ni vile vinavyohusiana na mmeng’enyo, vyanzo hivyo ni;
“Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori)
“Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu kama asprin, (NSAIDs), (Advil, Aleve, na zingine)
“Kuwa na mawazo mengi
“Kula vyakula vinavyozalisha acid kwa wingi
“Kunywa pombe na vinywaji vikali
“Uvutaji wa sigara
“Kuto kula mlo kwa mpangilio
MADHARA YA UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO
* Uvujaji wa damu ndani ya utumbo:
Hali hii yaweza kusababishwa na vidonda kuenea hadi kwenye mishipa ya damu na hivyo kufanya damu kuanza kuvuja. Hali hii ni hatari sana na inahitaji tiba ya dharura.
* Vidonda vya tumbo huweza kusababisha tundu (kutoboka kwa ukuta wa tumbo) na kufanya vitu vilivyo ndani ya utumbo kutapakaa katika tumbo (abdomen)
Hali hii huitwa peritonitis na ni hatari sana na inahitaji matibabu ya dharura. Aidha, kuenea huko kunaweza pia kuathiri tezi kongosho na kusababisha madhara katika tezi hiyo, ugonjwa unaojulikana kama pancreatitis.
* Vidonda vya tumbo vinaweza pia kuenea na kuathiri pia viungo vya jirani kama vile ini au kongosho (pancrease)
*Kuvimba kwa kuta za tumbo pamoja na makovu yanayosababishwa na vidonda hivi huweza kusababisha kuziba kwa njia ya kupitishia chakula kutoka kwenye tumbo (stomach) kwenda sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenum) hali ambayo kitaalamu huitwa gastric outlet obstruction.
* Iwapo vidonda vya tumbo vimesababishwa na H. pylori, kuna uwezekano wa kati ya mara tatu hadi ya sita ya mgonjwa kupata kansa ya tumbo (stomach cancer).
JINSI YA KUEPUKANA NA VIDONDA VYA TUMBO
🥑Kunywa maji mengi
Kila uamkapo asubuhi hakikisha unakunywa maji ya kutosha yasiwe ya baridi sana au ya moto.
Hakikisha maji unakunywa kabla ya kusafisha kinywa.
🥑Punguza mawazo, fanya mazoezi yatakayo kupunguza mawazo
Fanya kitu ambacho unaweza kuwa na furaha na Kusahau Mambo yote yanayokusumbua.
🥑Punguza (balansi) kiwango cha lehemu (choresterol)
Epuka vyakula vyenye mafuta mengi au vya kusindikwa viwandani
🥑Usivute sigara
🥑Punguza au acha kunywa pombe
🥑 Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali
🥑Lala vizuri kwa muda mzuri – masaa 7 hadi 9
MWONGOZO WA VYAKULA
Wewe unae teseka na vidonda vya tumbo Kuna vitu unavyo takiwa kuacha kutumia kabisa kwa Sasa ili uweze kuwa salama
Vitu usivyopaswa kuvitumia.
🔺Vyakula vya kusisimua mwili,
🔺Vyakula na VINYWAJI vyenye caffeine na Asidi nyingi mfano
🔺chai ya rangi,
🔺 kahawa,
🔺vyakula vya kwenye makopo soda na juice za viwandani hivyo huchangia kwa kiasi kikubwa vidonda vya tumbo lakini pia acha
kutumia chumvi nyingi hasa 🔺epuka kutumia chumvi mbichi epuka kutumia
🔺vilevi vya Aina yoyote,
🔺 karanga,
🔺dagaa,
🔺 Maziwa
🔺 maharage,
🔺kuku wa kisasa au mayai ya kisasa,
🔺pilau,
🔺nyama nyekundu
🔺 Sukari
🔺 chainise kisamvu , nk hivyo husababisha kwa kiasi kikubwa kutokupona kwa vidonda vya tumbo hivyo viache kwa mda mpaka utakapo pona
Matunda unaweza kupunguza na ikiwezekana Acha kabisa kutumia matunda yafwatayo
🔺 Nanasi
🔺 Chungwa
🔺Ukwaju
🔺 Chips
🔺Limao au ndimu
Vyakula unavyo weza kutumia
Penda kula matunda kwa kiasi kikubwa Sana kila unapo pata Chakula akikisha Kuna matunda pembeni yako, ,Penda kula
✅ ndizi za kupika au zilizo iva au unga wa ndizi pia itakusaidia,
✅ Parachichi
✅ Tikiti maji
✅Tango
✅Karoti
MBOGA ZA MAJANI
penda kula mboga za majani kama
✅mlenda,
✅Matembele,
✅mchicha,
✅kabeji,
✅nyanya chungu*
✅ BAMIA
Lakini unaweza kutumia samaki wabichi wa kuchemsha
CHAI YA ASUBUHI KWA MGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBU
Chai yako iwe na viungo Mbalimbali Kama vile
✅Tangawizi,
✅ mdalasini,
✅ iliki,
✅mchaichai,
✅Karafuu, Kumbuka viungo hivi vinaweza Kuwa vya unga au majani na unaweza kutumia vyote au ata kimoja Kama mazingiza hayaruhusu,
ANGALIZO 👉 Kumbuka hutakiwi kutumia vitu vyenye caffeine nyingi Usitumie majani ya dukani mfano chai Bora,
ANGALIZO HUTAKIWI KUTUMIA SUKARI wewe mwenye vidonda vya tumbo tumia asali badala ya sukari ,Tena asali mbichi ambayo haijachakachuliwa kumbuka asali Ni miongoni mwa dawa ya vidonda vya tumbo.
VITAFUNWA
👉Mayai ya kienyeji
👉mkate wa ngano ambayo haijakobolewa brown bread
👉Chapati ya unga wa Nagano amabayo haijakobolewa, ikiwezekana hizi chapati zikandwe na tui la nazi na sio maji tu
👉Ndizi za kuchemsha
👉Ndizi Nyama na Nazi
👉Viazi vitamu vya kuchemsha
👉Nyama ya kuku wa kienyeji na Nazi
👉 Wali Nazi
FANYA HIVI KILA ASUBUHI.
Chukua glass Yako weka maji safi na salama yasiyo ya moto, baridi sana Wala uvuguvugu…. Yawe MAJI ya kawaida
Unaweza kunywa glass Moja au nusu glass au zaidi Kila siku asubuhi
FAIDA YA KUNYWA MAJI ASUBUHI KABLA YA KUFANYA CHOCHOTE
- Kuondoa sumu mwilini
- Kupunguza uzito
- Kuondoa kiungulia na matatizo ya mmeng’enyo wa chakula
- Kupunguza uwezekano wa kupata bawasili maana inalainisha choo
- Kuboresha na kuimarisha ngozi
6.Kuongeza nguvu mwilini
7.Kupunguza maumivu ya vidonda tumboni

Wasilina nasi kama utahitaji tiba na msadaa zaidi





