Simba wanamtaka beki wa kati kutoka Asec Mimosas Anthony Tra Bi Tra
Mabosi wa Simba wameshatuma mtu kwa beki wa kati wa ASEC Mimosas, Anthony Tra Bi Tra (25). Hesabu za vigogo hao wa Simba zinakuja baada ya kutokuwa na uhakika wa kubakia msimu ujao kwa beki wa kikosi hicho, Henock Inonga ambaye taarifa zinaeleza mwishoni mwa msimu huu anaweza kuondoka ili kutafuta changamoto mpya huku FAR Rabat ya Morocco ikimuhitaji. .
Tra Bi Tra ameiongoza ASEC Mimosas kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku akionyesha nia ya dhati ya kutaka kuondoka kutafuta changamoto mpya baada ya kuitumikia timu hiyo tangu mwaka 2021 akitokea FC Foix. .
Tayari mabosi hao wameanza kujipanga mapema baada ya kuona ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu ni ngumu kuuchukua kwani watani zao Yanga wako kwenye nafasi nzuri ya kuuchukua kwa mara ya tatu mfululizo jambo ambalo hawataki litokea msimu ujao.
Simba mpaka sasa ina asilimia kubwa ya kumpata beki mzawa wa Coastal Union, Lameck Lawi mwenye uwezo wa kucheza nafasi tatu tofauti kuanzia beki wa kati, beki wa kushoto na kiungo wa kati jambo linalowafanya kuhamishia nguvu kwa nyota wa kigeni.





