Vita Vikali kati ya Elon Musk na Mtoto wake Vivian
Vita Vikali kati ya Elon Musk na Mtoto wake Vivian

Tajiri ElonMusk amemjibu Mtoto wake ambae alijibadilisha jinsia na kuwa Mwanamke baada ya kudai kuwa anampango wa kuondoka Marekani baada ya ushindi wa DonaldTrump kiti cha Urais.
Kupitia mtandao wa Threads Vivllainous aliandika.
“Nimefikiria hii kwa muda, lakini jana ilinithibitishia. Sioni mustakabali wangu kuwa Marekani. Hata kama atakuwa madarakani kwa miaka 4 pekee, hata kama kanuni za kupinga sheria hazitafanyika, watu ambao walipiga kura hii kwa hiari hawataenda popote hivi karibuni.”.
Baada ya Vivian kutangaza mipango yake ya kuondoka Marekani,Musk alijjbu kupitia X akili ya Mtoto wake wa Kiume Alishafariki itu ambacho Vivian alijibu jibu hilo kupitia Thread akimwambia Baba yake kuwa asimuingilie kwenye maamuzi yake.
Vivian ni mmoja ya watoto sita ambao Musk alipata na mke wake wa kwanza, JustineWilson. Alibadilisha jina lake kisheria mnamo 2022 na kubadilisha jinsia kitu ambacho Musk hakikumpendeza na akadai anamuhesabu kama amekufa kwake.






