50 Cent Aandaa Makala ya Kuanika Maisha ya P Diddy
50 Cent Aandaa Makala ya Kuanika Maisha ya P Diddy

Rapa 50 Cent ameweka wazi mpango
wake wa kutengeneza filamu inayochunguza tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia na ukatili zinazomkumba Sean “Diddy” Combs.
Akİzungumza kwenye kipindi cha GMA3:
What You Need to Know, 50 Cent alifafanua kuwa filamu hiyo inatayarishwa kwa wakati halisi, ikijumuisha matukio yanapotangazwa.
“Tunaingia katika mradi mgumu sana kwa sababu kila siku kuna tuhuma mpya zinazoibuka,” alisema. “Imegeuka kuwa kama pweza mwenye mikono mingi, na kuna
mambo mengi yanayoendelea.”
Filamu hiyo, inayoongozwa na Alexandria Stapleton, inalenga kuchunguza tuhuma hizi ambazo zimekuwepo kwa miaka kadhaa. 50 Cent alikiri kushangazwa na wingi wa madai dhidi ya Diddy, akisema, “Sikutegemea kuw
hali ingekuwa mbaya kiasi hiki.”
Wakati Diddy akisubiri kesi yake ya mashtaka ya ulanguzi wa binadamu na utapeli, 50 Cent amejitolea kufichua ukweli wa tuhuma hizi kwa mtazamo wake. Filamu hiyo ambayo bado haina jina rasmi, inatarajiwa kuwapa sauti wale walioumizwa.






