Abdulmajid Nsekelawamewahamasisha wanahisa kuhudhuria semina maalum itakayofanyika Ijumaa,tarehe 16,Mei 2025 na Mkutano mkuu wa wanahisa utakaofanyika Jumamosi,tarehe 17,Mei 2025 katika ukumbi wa AICC,Arusha.
Wakati Bado CRDB Bank inaendelea kusheherekea Miaka 30 ya kuwahudumia watanzania,Leo Bodi ya Body ya Wakurugenzi ikiongozwa na Mwenyekiti wake Dr. Ally Laay na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Bw Abdulmajid Nsekela katika mkutano maalumu na waandishi wa habari wamewahamasisha wanahisa kuhudhuria semina maalum itakayofanyika Ijumaa,tarehe 16,Mei 2025 na Mkutano mkuu wa wanahisa utakaofanyika Jumamosi,tarehe 17,Mei 2025 katika ukumbi wa AICC,Arusha.
Mgeni Rasmi atakayefungua Semina anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Philip Isdor Mpango .
Pia Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Bw. Abdulmajid Nsekela amesisitiza kuwa ni haki ya msingi na ya kisheria kwa wanahisa kuhudhuria semina na Mkutano mkuu.






