Act Wazalendo Wawaomba Chadema Wasitishe Maandamano Kesho
Act Wazalendo Wawaomba Chadema Wasitishe Maandamano Kesho.

Chama cha ACT Wazalendo kimekiomba
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kiahirishe maandamano yao ya September 23,2024 na pia wamneiomba Serikali na Polisi kuchukua hatua za
kupunguza joto na kutuliza hali ili kujenga
mazingira ya mazungumzo ya dhati yanayolenga kupata ufumbuzi sahihi wa mambo yote yanayolalamikiwa na
pande zote.
Taarifa iliyotolewa leo September 22,2024 na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Dorothy Manka J. Semu, imesema “Kwamba Tanzania inayo hazina ya Watu wenye busara na hekima wakiongozwa na Rais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan na Viongozi wetu wa Dini ambao wakifanya kazi pamoja wanaweza kututoa kwenye hali hii
iliyopo sasa na tukatoka tukiwa imara zaidi kama Taifa na hata kuwa mfano kwa wengine kama ilivyo historia yetu adhimu”
“Mimi binafsi na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Othman Masoud Othman tunafanya mazungumzo na pande zote mbili katika jitihada za kupata mwafaka wa hali tuliyo
nayo, tunaomba Watanzania wote tuungane katika hili”
“Kwamba tunatoa wito kwa pande zote kutuliza vichwa na kutoa nafasi kwa hekima na busara za uongozi ili zitumike kupata ufumbuzi na suluhisho muafaka”







