Sintogombea Tena Urais 2026, Museveni Mitano Tena Uganda
Sintogombea Tena Urais 2026,Museveni Tena Uganda
Mkuu wa Majeshi (CDF) wa Uganda, Jenerali
Muhoozi Kainerugaba ambaye pia ni Mtoto wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema amesitisha mpango wake wa kugombea Urais Nchini humo katika Uchaguzi ujao wa mwaka 2026 na badala yake ametangaza kumuunga mkono Baba yake Rais Museveni kuwa ndiye anastahili kuendelea kuwa Rais wa Nchi hiyo kwa mnuhula wa saba mfululizo.
Muhoozi amesema “Natangaza kuwa sitogombea Urais 2026, Mungu ameniambia niweke nguvu kwenye Jeshi lake kwanza, namuunga mkono Rais Museveni kwenye
Uchaguzi ujao, kwangu hakuna kitu kitakatifu zaidi Duniani kushinda Jeshi la Uganda, siwezi kufikiria heshima nyingine zaidi ya heshima ya kuwa ndani ya Jeshi la Uganda, Mungu libaliki Jeshi letu na uitakase
Uganda milele”
Katika hatua nyingine Muhoozi amesema “Hakuna Raia wa kawaida ataiongoza Uganda baada ya Rais Museveni kumaliza muda wake, Vyombo vya Usalama havitokubali hilo, Rais ajaye wa Uganda atakuwa Mwanajeshi au Polisi”
Itakumbukwa March 16,2023 Muhoozi alitangaza nia ya kutaka kumrithi Baba yake kiti cha Urais wa Uganda ambapo alisema atagombea Urais mwaka 2026 huku akisema inatosha sasa kuendelea kuongozwa na Wazee lakini siku chache baadaye Baba yake Rais Museveni akamjibu akisema Wananchi wa Uganda wataamua kama Mtoto wake Muhoozi anafaa kuwa Rais wa Nchi hiyo muda utakapofika ama laah na akaongeza kuwa Viongozi wa Uganda hawachaguliwi Twitter.
Kwa sasa Museveni anaiongoza Uganda kwa muhula wa sita mfululizo, hii ni baada ya kushinda uchaguzi wa January 14, 2021 kwa kuwashinda Wagombea wengine 10 katika nafasi ya Urais (akiwemo Robet Kyaluganyi maarufu Bobi Wine) kwa ushindi wa 58% na endapo atagombea tena mwaka 2026 itakuwa ni muhula wake wa saba mfululizo.