AFUNGWA NA MAHABUSU KUSIKILIZA KESI KWA MAHAKAMA MTANDAO NI KWA SABABU ZA KIUSALAMA: BASHUNGWA
đAtoa maelekezo kufuatia matamko ya CHADEMA.
đAsema hakuna âVIP treatmentâ kwa wanaotaka kuwaona Wafungwa na Mahabusu.
đAagiza Jeshi la Polisi kudhibiti maandamano na matishio ya kiusalama.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amesema kuwa Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania litaendelea kuwawezesha Wafungwa na Mahabusu kusikiliza mashauri yao wakiwa magerezani kupitia Mahakama Mtandao, hasa kunapokuwepo na viashiria vya matishio ya kiusalama, ili kudumisha amani na kulinda usalama wa raia na mali zao.
Ameeleza kuwa mojawapo ya sababu ya kuendelea kutumia Mahakama Mtandao ni masuala ya kiusalama, ambapo hivi karibuni baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wametoa matamko yanayoashiria uvunjifu wa amani na usalama, hali iliyosababisha baadhi ya Wafungwa na Mahabusu kusikiliza mashauri yao kwa njia ya mtandao.
Bashungwa ameyasema hayo leo, tarehe 30 Aprili 2025 jijini Dodoma, alipoambata na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), kukagua Makasha ya kisasa ya Mahakama Mtandao yanayowezesha usikilizaji wa mashauri kwa njia ya kiteknolojia katima Gereza la Isanga -Dodoma
âJeshi la Polisi linapokuwa na taarifa za kiinterejensia za wazi na zisizo wazi, kwa mfano maandamano ya CHADEMA na Watanzania ni mashahidi, Viongozi wa CHADEMA walisema waziwazi kwamba waandamana wakakinukishe. Jeshi linapokuwa na taarifa za kiusalama likashirikiana na Mahakama kutoa haki ile ile lakini kwa kutumia teknologia ya Mahakama Mtandao ili kuzuia fujo mtaani, naomba Watanzania watueleweâ amesema Bashungwa.
Aidha, Bashungwa amewahakikishia wananchi kuwa Vyombo vya Usalama vitaendelea kuhakikisha kuna utulivu kwa kudhibiti maandamano, matishio ya kiusalama, na vitendo vyote vinavyoweza kuhatarisha amani na usalama wa nchi.
âNiendelee kuliagiza Jeshi la Polisi kusimamia sheria na kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa na amani, hata yule ambaye hataki amani, sisi tutamlazimisha kuhakikisha nchi yetu inakuwa amani na salamaâ amesisitiza Bashungwa
Pia, Bashungwa ameliagiza Jeshi la Magereza kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa na amani, hata yule ambaye hataki amani, sisi tutamlazimisha kuhakikisha nchi yetu inakuwa amani na salamaâ amesisitiza Bashungwa